Tukakongamaneni

Kuhusu Kongamano Hili
Kuhusu Kongamano Hili
Kutana na wataalamu, wakereketwa, na wadau wa Kiswahili toka sehemu mbalimbali Duniani. Utafurahi kutangamana na Waswahili wengine na kuwa sehemu ya familia kubwa ya wasemaji wa Kiswahili Duniani! Mada kuu ni “Kiswahili na Lugha Nyingine za Kiafrika katika Zama za AI: Fursa na Changamoto.“ Jioni ya tarehe 16 Disemba, kutakuwa na tamasha kubwa la Utamaduni wa Mswahili, ambapo watu wote wanakaribishwa, hata wale ambao hawakushiriki katika kongamano.
Kamati ya maandalizi inaangalia uwezekano wa kuandaa shughuli za kitalii. Wale watakaohitaji kushiriki katika utalii watajulishwa gharama zitakuwa kiasi gani na ni maeneo gani ya kiutalii yatakayotembelewa.